History
Icon-add-to-playlist Icon-download Icon-drawer-up
Share this ... ×
...
By ...
Embed:
Copy
Intro Doc - Masomo ya Msingi
Clean
May 06, 2012 04:31 AM PDT
itunes pic

Maono ya kanisa la nyumba kwa nyumba – (Home Church Vision)

Mkakati

Viongozi watafundishwa vipindi saba vya mafundisho kutoka kwenye ya “Mafundisho ya Misingi” (Foundations), kwa siku moja au mbili, na baada ya hapo kanisa la nyumba kwa nyumba hufundishwa vipindi hivyo saba kwa muda wa majuma saba ikiwa ni somo moja kwa kila juma (kiongozi ndiye anyeongoza). Katika juma la nane ubatizo wa wazi huandaliwa kwa ajili ya waliokoka wapya ha hii huwa ni fursa ya kuwapata watu wengine kwa ajili ya awamu nyingine ya “Mafudnisho ya Misingi” kwa ajili ya makanisa mapya ya “nyumba kwa nyumba”.

Wakati huo huo, lile kanisa la kwanza la nyumba kwa nyuma huingia katika majuma saba ya kozi fupi ya kutoka Kozi ya kusoma Biblia kwa Njia ya Roho (The Way of the Spirit Bible Reading Course), kwa mfano “Onyesho la njia ya Wokovu” (The Drama of Salvation). Katika Juma la saba kunakuwa na ubatizo mwingine wa wazi (au tukio la wazi linalofanana nalo), ambapo awamu ya tatu ya Kanisa la Nyumba Kwa nyumba inaanzishwa.

Lile kundi la kwanza la kanisa la nyumba kwa nyumba sasa huingia kwenye mafundisho mapya ya Mafundisho kwa Uzima (Training For Life –TFL) kwa ukamilifu, huku kundi la pili likiingia kwenye “Onyesho la njia ya Wokovu” (au somo linalofanana nalo) na lile la tatu huingia kwenye mafundisho saba kutoka kwnye ya “Mafundisho ya Misingi” (Foundations). Na hivyo kuendelea katika mfumo huo huo….

Kumbuka kwamba kwa kila kanisa la nyumba kwa nyumba kiongozi ni lazima awatafute watu wenye uwezo wa kuongoza ili kumsaidia na kuongoza Makanisa Mapya ya nyumba kwa nyumba yanayoanzishwa.

Hatimaye lile kanisa la kwanza linakuwa Waangalizi wa Kitume kwa ajili ya makanisa wanayoyasimamia, na kutenda kazi pamoja na Waangalizi wengine wa Kitume, na baadhi ya hawa watakuwa kwenye Timu ya Kitaifa ya Waangalizi wa Kitume wanaokusaidia, kama Kiongozi Mpakwa Mafuta, unayesimamia kazi ya kitaifa.

Kuna kazi nyingi kwa kila aliye kwenye timu hiyo, kwa jinsi Mungu anavyowaoongoza ni muhimu . . . .

Itakuwa vizuri kusikia watu wanasemaje juu ya kukua kwa makanisa haya ya anyumba kwa nyumba. Kumbuka umuhimu wa kuwa na timu ‘iliyoitwa na kupakwa mafuta’ kutenda kazi na kiongozi wa huduma. Kazi itakuwa kubwa mno kwa mtu mmoja peke yake.

Viongozi, tafuta watu ambao watatokana na wewe mwenyewe na kukua katika Kristo. Wewe una upako wa kitume lakini kumbuka kwamba wao hawana. Kila aliye kwenye timu atakuwa na kazi ya kufanya chini ya ulezi wako lakini hakuna mtu mmoja awezaye kufanya kazi unayoifanya, kwa hiyo tafuta timu ya watu ambao watakuwa na majukumu katika maeneo maalum ya upako wako …. Kwa mafano mchungaji, mwalimu, muinjilist, na nabii. Pia utahitaji wasimamizi wa shughuli za kiutawala waliotiwa mafuta na walio na karama za masaidiano (kuendesha, kupika, kufanya kazi mbalimbali; (hawa watakuwa mashemasi).

Mpangilio wa huduma unatakiwa kuwa namna hii….

Mch Peter (Timu ya TheWayCM) >Kiongozi wa Kitume wa Kitaifa na timu yake (timu hii itajumuisha wazee kutoka majimbo mabimbali)> Wasimamizi wa makanisa ya nyumba kwa nyumba (wazee) na wasidizi wao (mashemasi) kutoka kila jimbo > washirika

Masomo ya Msingi 1 - Kuwa Mwana wa Mungu
Clean
May 06, 2012 04:35 AM PDT
itunes pic

1. Kuwa Mwana wa Mungu

1) Unadhani ni kwa nini Mungu alichagua kumtuma Yesu ulimwenguni?
2) sasa tunaweza kumwita Mungu baba nasi watoto wake. Inamaanisha nini wewe kuwa mwana wa Mungu’?
3) Ikiwa ‘dhambi’ inamaanisha tunatengwa na Mungu, ni nini kinachoturejesha kwa Mungu?
4) Petro anasema tunatakiwa kujazwa na kuongozwa na Roho Mtakatifu’. Unadhani ana maana gain kwa kusema hivyo?
5) Kusudi la wokovu wetu ni nini?
6)Kama ukiulizwa kueleza maana ya ujumbe wa Habari Njema/Injili utaelezaje?

Kibali kimetolewa kutengeneza nakala kivuli za masomo haya na kuyatumia kwa ajili ya kujifunza na si biashara.

Masomo ya Msingi 2 - Ubatizo katika Roho Mtakatifu
Clean
May 06, 2012 04:37 AM PDT
itunes pic

2. Ubatizo katika Roho Mtakatifu

1)Yesu alifanya nini kwa ajili yetu pale msalabani?
2) ‘Ubatizo wa Roho Mtakatifu” unaelezwa kwamba ni karama. Ni kwa njia gani unafikiri ni karama?
3) Kama ilivyo kwa ‘karama’ yoyote toka kwa Mungu, ni lazima tuwe na shauku na kiu ya ‘Ubatizo wa Roho Mtakatifu’ ni kwa kiasi ganui wewe unahitaji karama hii?
4) Roho Mtakatifu wa Mungu huionda hofu. Je wewe una hofu yoyote na kama ipo utaishughulikiaje?
5) Mungu anatufanya ‘viumbe vipya’. Je unajisikia kuwa kiumbe kipya katika maisha yako ya Kikristo na ni nini kinacholeta tofauti hii katika maisha yako?
6) Roho Mtakatifu ni nguvu ya Mungu kwa ajili yetu ya kutuwezesha kuifanya kazi yake hapa duniani na kumfuata Yesu. Ni kwa njia gain Roho Mtakatifu hutusaidia kumfuata Yesu?

Kibali kimetolewa kutengeneza nakala kivuli za masomo haya na kuyatumia kwa ajili ya kujifunza na si biashara..

Masomo ya Msingi 3 - Kunena kwa lugha mpya
Clean
May 06, 2012 04:38 AM PDT
itunes pic

3. Kunena kwa lugha mpya

1) Petro anasema ‘kushuhudia ndio maisha yetu’. Matendo yana sauti zaidi ya maneno. Ni kwa njia gain wewe unashuhudia?
2) ’Kunena kwa lugha mpya mnenaji‘.
Unaelewa nini kwa maneno haya?
3) Kama umewahi wewe mwenyewe ‘kunena kwa lugha’’, ulijisikiaje ulipomsikia Petro akinena na kuimba katika lugha?
4) Huwezi kujua kukimbia kabla ya kutembea. Unahitaji kupokea ubatizo katika Roho Mtakatifu kabla hujaweza kusema na Mungu kwa lugha hii. Kwa nini?
5) ‘Unaponena na kuimba katika Roho Mtakatifu, nguvu hii kutoka kwa Mungu huwafikia wale wanaokuzunguka’. Unadhani kunena kwa lugha kuna umuhimu gani katika kushuhudia kwetu?
6) Je umeyaona mafundisho haya, na yale yaliyotangulia kuwa ya msaada katika ufahamu wako juu ya Roho Mtakatifu na Kunena kwa lugha na kama hivyo ndivyo kwa namna gani?

Kibali kimetolewa kutengeneza nakala kivuli za masomo haya na kuyatumia kwa ajili ya kujifunza na si biashara..

Masomo ya Msingi 4 - Urafiki wa karibu na Mungu
Clean
May 06, 2012 04:40 AM PDT
itunes pic

4. Urafiki wa karibu na Mungu

1) Ikiwa ‘unasikia kutoka kwa Mungu’, Je anakuambia nini?
2) ’Yesu alikuja kutuonyesha ‘njia’ ya kuishi. Je kulikuwa na umuhimu gani kwa Yesu kutuonyesha njia kwa matendo, na hii ina maana gani kwako?
3) Unapookoka je inawezekana kukutana na Mungu kwa njia iliyo binafsi, na ya katibu kabisa kila siku. Je hivi ndivyo ilivyo kwako?
4) Je tunaupataje urafiki wa karibu kabisa na Kristo?
5) Je ndoto na maono vina umuhimu gain katika uhusiano wetu na Mungu?

Kibali kimetolewa kutengeneza nakala kivuli za masomo haya na kuyatumia kwa ajili ya kujifunza na si biashara.

Masomo ya Msingi 5 - Kuingia ndani ya Yesu
Clean
May 06, 2012 04:41 AM PDT
itunes pic

5. Kuingia ndani ya Yesu

1) Ni nini kinachomfanya Mungu , kuwa Baba yetu ‘Mwema’? Na je tunawezaje kupokea vitu ‘vyema’ kutoka kwake (zile shauku za mioyo yetu) ?
2)Unaelewa nini juu ya ‘kuwa ndani ya Kristo yesu’?
3) Yesu alisema, ‘Bali utafuteni kwanza Ufalme wa Mungu’. Kwa nini jambo hili ni la muhimu sana?
4) Tunawezaje kumpinga ‘shetani’?
5) ‘Unyenyekevu kwa Mungu unahusisha sisi kujisalimisha katika ushindi wa Mwanawe‘. Je ukweli huu unawezaje kutupa ujasiri wa kumkaribia Yesu tunapomfuata?
6) ’Yeyote atakeye kunifuata ni lazima ajitwike msalaba wake’. Je kuubeba ‘msalaba’ kuna maana gain kwetu?

Kibali kimetolewa kutengeneza nakala kivuli za masomo haya na kuyatumia kwa ajili ya kujifunza na si biashara.

Masomo ya Msingi 6 - Udanganyifu
Clean
May 06, 2012 04:44 AM PDT
itunes pic

6. Udanganyifu

1) Kuna umuhimu gani kwetu kunyenyekea kwa Mungu na kutofuata vitu vya ulimwengu huu?
2) Yesu alipewa mamlaka yote. Je unadhani kuna uwezekano wa kuwa na mamlaka katika maisha yetu, na kwa namna gain? ( )
3) Shetani hutudanganya kutenda dhambi, kwa kutushawishi kwa vitu vinavyotamanisha.
‘Udanganyifu huu ni uongo uliofichika huku ukionekana kama kweli’
Je umewahi kudanganyika, na je unaweza kueleza ulivyotokea?
4) Ni kwa nini ni muhimu kwa fahamu zetu kuelekezwa kwa Kristo?
5) Watu wengi leo wanatafuta ‘ufahamu’, kama ilivyokuwa kwa Wayunani nyakati za Paulo. Wanatafuta tu kujaza akili zao (kutoka kwenye mti wa ujuzi), badala ya moyo na akili (mti wa uzima). Kwa nini hiki ni kitu cha hatari?
6) Petro anaielezea mikusanyiko ya watu kama makanisa bandia’.
Je unaelewa alimaanisha nini kwa maneno hayo?

Kibali kimetolewa kutengeneza nakala kivuli za masomo haya na kuyatumia kwa ajili ya kujifunza na si biashara..

Masomo ya Msingi 7 - Kuenenda katika Nuru
Clean
May 06, 2012 04:45 AM PDT
itunes pic

7. Kuenenda katika Nuru

1) Ulimwengu unachukia ‘Nuru ya Ulimwengu’. Kwa nini?
2) Petro alieleza kwa jina la Yohana maana yake ‘mpendwa’. Je unajua maana ya jina lako, na je unadhani linakuelezea wewe ulivyo?
3) Jinsi tunavyoishi ndiyo injili tunayoihubiri. Mara nyingi Biblia inaitwa ‘Maneno ya Uzima’. Kwa nini unafikiri hivi ndivyo?
4) Kwa nini kuungama ‘ni kitu chema kwa nafsi’? Na kwa nini ni vigumu sana kwetu kusema ‘samahani’?
5) Nuru hutuangazia njia kule tuendako ‘Njia kuu ya Utakatifu’
( ) Je uko katika njia kuu ya Utakatifu?
6) Kwa nini ni muhimu ‘Kutembea katika Nuru’?

Kibali kimetolewa kutengeneza nakala kivuli za masomo haya na kuyatumia kwa ajili ya kujifunza na si biashara..